KARIBU NG'S_CLINIC

MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE...?

 














MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE? 


Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX

Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY

Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana

Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana.


FAHAMU SIFA ZA CHROMOSOMES X Na Y ZA MWANAUME

Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto. 


SIFA ZA CHROMOSOMES Y 


1.Zina spidi  kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe  zitawahi kwenda kurutubisha

2.Zina maisha mafupi sana kulinganisha na X 


SIFA ZA CHROMOSOMES X 


1.Zina spidi ndogo sana 

2.Zina maisha marefu kulinganisha na Y 

Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndo zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka. 


MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA JINSIA 


1.Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya 1-28

2.Lazima mzunguko wako uwe na mpangilio sahihi(unaweza ukachunguza mzunguko wako kwa miezi minne mfululizo)

3.PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi 4-5.5(Tumia neplily pad kwa kuwa na PH sahihi

4.Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume 


JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME 


Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14

Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anaingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na ukikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnashiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kupata mtoto wa kiume 


KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI YAI LIMETOKA ILI KUPATA MTOTO WA KIUME?

Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ina spidi kubwa sana ni nyepesi na haiwezi kisihi mda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana ake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume 


JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE 

Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike utatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka  yani hapa ni baada ya kujua mzunguko

KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA SIKU TATU KABLA

Hii ni kwasababu  chromosome X ambazo ndo zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai 


KUNA BAADHI YA WAZEE WA ZAMANI WANAAMINI HAYA KATIKA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA. 


KUPATA WA KIKE

Kula samaki ,mboga za majani,matunda,bidhaa za maziwa,mbegu za matikiti majia na alzeti nk

Wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanamke akae juu nk 


KUPATA WA KIUME 

Kula nyama, ndizi ,Vyakula vya chumvi kama chips ila usizidishe chumvi,karanga na vyakula vingine vya potassium na sodium

Chromosomes Y zinahitaji pH ya alkane kuliko asidi ndio maana wazee waliona hili

Kuna mengi kuhusu wazee wa zamani ila nmeongelea haya ya mlo kwa maana yana mantiki kibaiolojia 


MAMBO YANAYOWEZA ATHIRI KUPATA MTOTO UNAYEMTAKA

1.Kushindwa kuhesabu siku.

2.Mzunguko mbovu wa hedhi.

Post a Comment

0 Comments