Fanya Mazoezi ya Mwili                                  Zoezi ni jambo lolote linalohusisha misuli na kusababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kasi ya kupumua. Kiwango kinacholeta faida ni mazoezi yasiyopungua dakika 30 kwa siku angalau siku tano kwa wiki.Imeandikwa kila mtu atakula kwa jasho lake,hivyo hakikisha unatoka JASHO angalau dakika 150 kwa wiki.

Mifano ya mazoezi ya kujishughulisha,  ni pamoja na:
●Kutembea, kukimbia taratibu, kuruka Kamba, kuendesha baiskeli, kunyayua vitu
vizito, kunyosha na kukunja, viungo pale ulipo, michezo mbalimbali ya uwanjani, Kucheza dansi huleta raha, hupunguza msongo wa mawazo na ni zoezi zuri.

Faida za mazoezi na kujishughulisha ni:
✅ Kudhibiti sukari na mafuta yaliyozidi mwilini.
✅Kuepusha shinikizo kubwa la damu,kisukari, magonjwa ya moyo na saratani.
✅Kuboresha mzunguko wa damu mwilini kwa afya ya mifupa na misuli.
✅ Kujenga misuli ambayo husaidia kutumia nishati ya ziada na hivyo kuepuka unene.
✅ Kupunguza unene na uzito wa ziada.
✅ Kupunguza msongo wa mawazo na kuwezesha usingizi mnono.
✅ Kusafisha nyumba na kufanya kazi nyingine za ndani au bustani.
✅ Kutembea kwenda safari fupi badala ya kutumia gari.
✅Kupanda ghorofa kwa kutumia ngazi badala ya lifti.
✅ Kuegesha gari mbali kidogo na ofisi ili kupata nafasi ya kutembea.
✅ Kufuatilia shughuli kwa kutembea badala ya kupiga simu kwa mtu uliye naye katika jengo moja.
✅Kufuatilia mwenyewe kwa kutembea badala ya kutuma.
✅Epuka Msongo wa Mawazo; kuwa na mawazo mengi huweza kuleta mfadhaiko unaoweza kujidhihirisha kwa:
● kuumwa kichwa.
● kukosa usingizi.
●kukosa hamu ya chakula.
●kukosa hamu ya kufanya shughuli yoyote hata mazoezi.
●unywaji wa pombe kuzidi kipimo.
●utumiaji wa tumbaku na madawa ya kulevya.
●Msongo wa mawazo huongeza uwezekano wa kupata shinikizo la damu na kisukari.

Mambo ya kufanya unapojisikia uchovu na msongo wa mawazo:
✅ Fanya mazoezi na shiriki katika shughuli za kijamii, michezo, tamasha, harusi, n.k.
✅ Panga kazi zako za siku na usijitwike mzigo usio wako au usiouweza.
✅Jadili matatizo na mtu unayemuamini na Pumzika vya kutosha.