KARIBU NG'S_CLINIC

TATIZO LA UJAUZITO/MIMBA KUHARIBIKA...✍️

 

TATIZO LA UJAUZITO/MIMBA KUHARIBIKA...✍️....?✍️......?✍️......?✍️....?

(MISCARRIAGE).
Kuharibika kwa ujauzito ni hali inayotokea ambapo ujauzito (mimba) hutoka (hufikia ukomo) wenyewe kabla ya wiki ya 28 (miezi saba) ya ujauzito.

Kwa kawaida kipindi cha ujauzito kimegawanyika kwa vipindi vitatu yaani, miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) , miezi mitatu ya kati (2nd trimester) na miezi mitatu ya mwisho (3rd trimester).

Mimba nyingi huaribika kipindi cha wiki 13 (miezi mitatu) za mwazo. Sababu kubwa kwa mimba kuharibika kipindi hiki inaweza kuwa ni mapungufu katika vinasaba (chromosomal abnormality).

SABABU ZINGINE ZA UJAUZITO KUHARIBIKA;

1. Matatizo ya vichocheo (hormonal problems).
2. Maambukizi (infections) mfano U.T.I na P.I.D
3. Afya ya mama mjamzito.
4. Uvutaji wa sigara.
5. Matumizi ya pombe na madawa.
6.umri wa mama mjamzito ( chini ya miaka 18 au juu ya miaka 45).
7.kupata ajali.
8. Makundi ya Damu (Rhesus incompatibility)

Mambo yafuatayo hayajathibitishwa kusababisha kuharibika kwa ujauzito.
1. Kufanya mapenzi ukiwa mjamzito.
2.kufanya kazi (ambazo sio hatarishi kwa ujauzito).
3.kufanya mazoezi ya wastani.

DALILI ZA UJAUZITO KUHARIBIKA.

1. maumivu ya wastani au makali ya tumbo na mgongo ( maumivu ni makali zaidi ya maumivu ya wakati wa hedhi).
2. Kupungua uzito.
3. Kutokwa na ute mweupe ( kama makamasi) au pink ukeni.
4. Kutokwa na damu nyepesi nyekundu au kahawia (brown) ukeni.
5. Kutokwa na mabonge ya damu ukeni.
6. Kupotea gafla kwa dalili za ujauzito.

Tafadhali, kama ukipata mojawapo ya dalili hizo ni muhimu kuwaona wataalamu wa afya ili kujua hali ya ujauzito wako.


Fanya yafuatayo kuzuia au kujikinga na kuharibika kwa ujauzito.

1.fanya mazoezi ya wastani.
2.zingatia lishe bora.
3.jizue kuwa na msongo wa mawazo.
4.usivute sigara na usikae karibu na mtu anayevuta sigara.
5.usinywe pombe.

UNASHAURIWA, kukaa miezi sita baada ya kupata tatizo la kuharibika kwa ujauzito ,ndipo upate ujauzito mwingine.

Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi..

Post a Comment

0 Comments