Ni aina ya maumivu ya kifua yanayatokea baada ya kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye moyo. Kupungua kwa mzunguko wa damu husababisha kukosa hewa safi ya oksijeni kwenye moyo.


Maumivu hutokea baada ya mwili kufanya kazi flani ama pale unapopata msongo wa mawazo.
Mumivu haya ya chembe moyo husababisha mtu kukosa raha, kuhisi kama kifua kimejaa na kubana kwa kifua eneo la katikati.

Chembe Moyo Hutokea Wakati gani?

Chembe ya moyo hutokea pale misuli ya moyo inapohitaji damu ya kutosha zaidi kuliko kawaida. Mfano wakati unafanya mazoezi, au unapokuwa na msongo wa mawazo. Unapokua umetulia mfano umekaa kwenye kitu kiwango cha hewa ya oksijeni kinachohitajika ni kidogo. Lakini unapokuwa kwenye shughuli kama kupanda mlima au kukimbia moyo unahitaji kiwango kikubwa cha hewa na ndio matokeo ya chembe moyo.

Dalili za Chembe Moyo
Pamoja na maumivu na kubana kwa kifua dalili zingine za chembe ya moyo ni kama

● Kushindwa kupumua vizuri

● Kupata kichefuchefu
Mwili kukosa nguvu na kupata ganzi

● Kutokwa na jasho na
Msongo wa mawazo

Mazingira na tabia Hatarishi Zinazopelekea kupata Chembe moyo
○ Kuwa na uzito mkubwa na kitambi

○ Kuwa na historia ya kugua magonjwa ya moyo

○ Kuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol au shinikizo la damu kuwa juu

○ Mgonjwa wa kisukari
Uvutaji wa sigara

○ Kutofanya mazoezi au kushugulisha mwili

○ Kula mlo mkubwa na
Mazingira ya joto kali au baridi kali

KWA HUDUMA/TIBA ZETU ZA UHAKIKA WASILIANA NASI KWA:
whatsapp/piga
+255758077020 👈🏼
        Au
+255622198368


[  ] 《Tunajali Afya Yako...Karibu Sana》□