KARIBU NG'S_CLINIC

🅾️ MATATIZO YA HEDHI YANAYO SABABISHA UGUMBA KWA MWANAMKE ⭕


 🅾️  MATATIZO YA  HEDHI YANAYO SABABISHA  UGUMBA KWA  MWANAMKE ⭕

___
🪄➡️ Ugumba kwa mwanamke ni hali ya mwanamke kushindwa kubeba ujauzito wakati huo akishiriki tendo la ndoa na mwenzi wake ambaye ana afya bora ya uzazi kwa zaidi ya mwaka mzima. 🪄

*❇️‼️ Ugumba una vyanzo vingi leo tutaangalia matatizo ya hedhi ambayo mwanamke akiyaona ni vema akachukua hatua mapema ili aepukane na tatizo la ugumba.*

➡️ Baadhi ya matatizo ya hedhi yanayoweza kusabaisha mwanamke akashindwa kubeba ujauzito:

*➢ 〽️Kutopata hedhi,* kwa kawaida kila mwezi mwanamke huingia katika siku zake za hedhi, ikitokea mwanamke anaona siku zinakwenda na haoni siku zake na hana ujauzito ni vema akachuka hatua za haraka ili ajue sababu za kukosa hedhi mapema.

*➢ 〽️Hedhi kuvurugika,* kila mwanamke anatakiwa kuwa na mzunguko maalum wa siku zake ambapo kwa kawaida huanzia siku 21 mpaka siku 35 japo wanawake wengi huwa na mzunguko wa siku 28.

🔈Ikitokea mwanamke anakaa miezi miwili ndio anaona hedhi au kila baada ya wiiki anaona hedhi si dalili njema kwa afya ya uzazi.

*➢〽️ Hedhi kutoka kidogo sana,* kuna baadhi ya wanawake huona damu ya hedhi matone machache tu na inatoka chini ya siku tatu. Wengi huona kama wanaepukana na usumbufu wa kubadili pedi hivyo huchukulia ni hali ya kawaida. Hii pia si dalili njema.

*➢ 〽️Hedhi nyingi sana,* mwanamke ambaye anatokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi kiasi ambacho anabadili pedi zaidi ya tatu kwa siku na inatoka kwa muda mrefu zaidi ya siku saba hii nayo si dalili njema.

*➢ 〽️Maumivu makali wakati wa hedhi,* kuna baadhi ya wanawake hupata maumivu makali kiasi cha kulazwa na kushindwa kuendelea na majukumu yao ya kila siku, hali hiyo ni kiashiria cha matatizo katika mfumo wa uzazi.

*JE,UNA DALILI ZOZOTE KATI YA HIZI HAPO JUU?🤔🤔*

🌹Inawezekana Ukawa Una Changamoto yoyote Ya Uzazi au Ya Kiafya na umehangaika kutafuta suluhisho la kudumu.
Usikate Tamaa.
Wasiliana nasi kwa simu namba;
+255758077020
          Au
+255622198368

Post a Comment

0 Comments