*Je unawezaje  kuzuia U.T.I?*

Kuna hatua mbalimbali ambazo zikichukuliwa zinaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya UTI.

Njia kuu ya kuzuia maambukizi ya njia ya mkojo ni pamoja na kuacha kutumia vipodozi, mafuta, losheni, manukato, kemikali na vitu vingine kusafisha sehemu za siri.


Hatua mbali mbali ambazo zikichukuliwa zinaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya UTI:

✅Kunywa maji mengi na uende haja ndogo mara kwa mara ili kusafisha njia ya mkojo.
✅Epuka vinywaji kama vile pombe na kahawa ambavyo vinaweza kudhuru kibofu.
✅Nenda haja ndogo mara baada ya kufanya tendo la ngono.
✅Jipanguse kuanzia mbele kwenda nyuma baada ya haja kubwa.
✅Hakikisha sehemu zako za siri ni safi kila wakati.
✅Kuoga kwa maji yanayotiririka( showers) ni bora zaidi na epuka kutumia mafuta.
✅Pedi (sodo) zinazotumiwa nje ni bora zaidi kuliko zile zinazoingizwa ndani
✅Epuka kutumia bidhaa za manukato katika sehemu ya siri.👇
✅Vaa nguo ya ndani(chupi) iliyotengenezwa kwa pamba na nguo ambazo hazikubani ili kuhakikisha sehemu zako za siri zinakua safi na kavu.

*NOTE: Watu wanashauriwa kuwasiliana na madaktari ama watalamu wa Afya wa matatizo ya  Uzazi ya wanawake iwapo atahisi kuwa na za UTI, hususan kama wana uwezekano wa kupata maambukizi ya figo.*

Matatizo haya yanahitaji uchunguzi na matibabu ya  haraka sana ili kuzuia hatari ya mwanamke kuwa MGUMBA.

Matibabu yatatolewa kwa muujibu wa chanzo husika ila mara nyingi huwa ni matitabu ya kurekebisha homoni (Program 1).