Vidonda vya tumbo(Peptic Ulcer)

Ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali kuyeyusha chakula unaoitwa mucus.

*CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO*

✅Bacteria waitwao Helicobacter pylori

✅Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin

✅Matumizi ya pombe na vinywaji vikali

✅Kuwa na mawazo mengi.

*DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO*

✅Kupata maumivu ya tumbo yanayokua kama moto(kuunguza) baada na kabla ya kula

✅Kupatwa na kiungulia karibu na chembe  ya moyo

✅Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa

✅Kichefuchefu na kutapika(wakati mwingine kutapika damu)

✅Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito

*MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO*

✅Saratani ya tumbo(Stomach Cancer)

✅Upungufu wa damu(Anemia)

✅Kuvuja kwa damu ndani ya mwili(Internal bleeding)

✅Kupungua kwa nguvu za kiume