KARIBU NG'S_CLINIC

*JE, UNAJUA VYANZO, DALILI NA MADHARA YA FANGASI SEHEMU ZA SIRI?*

 


*JE, UNAJUA VYANZO, DALILI NA MADHARA YA FANGASI SEHEMU ZA SIRI?*


*Je, Maambukizi Ya Fangasi Ni nini?*

Candida albacans ni vimelea wa fangasi ambao hukua kama fangasi ama seli zenye kusababisha kuwepo kwa maambukizi ya fangasi kwa mwanadamu.

Fangasi ya asili ijulikanayo kama Candida albicans, mara nyingi husababisha aina hii ya kuvimba kwa uke(Vaginitis). Kama inavyokadiriwa kuwa katika wanawake wanne, basi watatu wanaweza kuwa na maambukizi ya fangasi katika maisha yao,  haijalishi una umri gani. Hapo awali ilionekana kuwa jambo la kawaida sana mwanamke kuwa na maambuki ya fangasi sehemu za siri, lakini leo inaonekana kuwa tatizo la kutisha kwanai linaweza kuzarisha madhara mengine makubwa ambayo muhusika hakutarajia kama vile kuvimba ukeni, muwasho na masumbufu mbalimbali.

Magonjwa ya maambukizi yamekuwa yakienea kwa njia mbalimbali hasa kwa njia ya kujamiiana. Kwa upande mwingine maambukizi haya sio kwamba ni magonjwa ya zinaa tu. Wagonjwa wamekuwa wakipatwa na masumbufu mengi katika kutibu maambukizi katika via vya uzazi hasa fangasi.

*Je, Fangasi Inaambukizwaje?*

Mbali na kusababisha maambukizi ya fangasi sehemu za siri, fangasi pia husababisha maambukizi katika sehemu za mwili wako zenye unyevunyevu, kama vile mdomo(thrush), sehemu za kwapa, na sehemu za makucha. Vimelea wa fangasi pia wanaweza kusababisha tatizo la harara. Mambo yanayoongeza vihatarishi vya ugonjwa huu ni pamoja na;

🔸Matumizi ya madawa makali kama vile ya antibiotic, nk;

🔸Kisukari cha muda mrefu,

🔸Mabadiriko ya homoni, hasa kwa kina mama wenye ujauzito.

🔸Vidonge vya kupachika sehemu za uke,

🔸 Mavazi ya ndani yenye kubana sana, nafikiri kina dada mnaosoma makala hii hapo mlipo mumeshatambua maana najua hata sasa wapo wengi wenye mazoea ya kuvaa nguo za kubana ambazo wengi wanaita “Skin Tight”!

🔸Kutokuwa na usafi sehemu za uke

🔸Matumizi ya sabuni kwa kuoshea sehemu za uke sio kwamba zinasababisha fangasi bali zinaongeza hatari ya kupata maambukizi ya fangasi.

*Je, Dalili  Za Maambukizi Ya Fangasi Ukeni ni zipi* ?

Kama tulivyowahi kujifunza, dalili za maambukizi ya fangasi huwa kama ifuatavyo:

✅Kuhisi muwasho sehemu za uke
Kutokwa na uchafu wenye rangi nyeupe kama maziwa mtindi lakini hauna harufu.
Lakini wakati huohuo huwa kuna dalili zingine za kawaida pamoja na madhara ya fangasi. Kuongezeka kwa dalili hutegemeana na tatizo kukaa muda mrefu bila kupata tiba. Kwa upande mwingine napenda niseme hivi, tatizo la fangasi ukiwa unaritibu lakini linaendelea kujirudia mara kwa mara kwa muda mrefu, laweza kusababisha madhara makubwa. Hii ndio maana yafaa kumuona daktari wa vipimo haraka sana ikiwa kama utaona dalili zifuatazo kama vile;

✅Kuhisi hali ya kuwaka moto sehemu za uke

✅Kuhisi hali ya muwasho

✅Kutokwa na uchafu sehemu za uke hata kama ndio umeanza kutoka haijalishi ni mwingi au kidogo maana ndio dalili zenyewe za fangasi. Kumbuka kwa upande mwingine dalili hizi zaweza kuwa majimaji yenye harufu.

✅Kuhisi Maumivu wakati wa kujamiiana

✅Kuona hali ya uvimbe

✅Vidonda ama michubuko sehemu za siri.

Post a Comment

0 Comments